Habari za Afya

Sababu za kutumia madawa ya kulevya

Post hii inahusu zaidi sababu zinazopelekea mtu au kundi la watu kutumia madawa ya kulevya

Matumizi ya madawa ya kulevya yanaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwemo sababu za moja au zisizo za mojawapo kwa moja au wati wengine wanajiingiza kwa kujua au kwa kutojua kwa kadri tutakavyoona hapo kwa maelezo ya hapo chini.

 

1. Sababu za kimarika.

 Kuhusishwa na watu wanaotumia madawa kulevya kunaweza kusukuma mtu kujaribu ili akubalike katika kikundi au jamii fulani kwa sababu ya kimikumbo inawezekana kuwa vyuoni,mitaani au sehemu mbali mbali hasa kwa vijana.

2. Matatizo ya kisaikolojia na kijamii kwa ujumla.

 Watu wengi hujaribu kukabiliana na mfadhaiko, wasiwasi, unyogovu au kiwewe cha kihisia kwa kutumia madawa, baada ya watu kupata matatizo mbali mbali ilu kuweza kukubaliana na matatizo hayo upelekea kutumia madawa ya kulevya,kwa sababu hayo matulizo  huwa siyo ya kudumu na huwa ni ya mda watumiaji kuendelea kutumia mara kwa mara na baadae hali hiyo inakuwa sehemu ya maisha.

3. Ukosefu wa ajira na kutojishughulisha.

Kutokuwa na ajira  au kushindwa kujishughulisha ni njia mojawapo ya kuanza kutumia madawa ya kulevya kama burudani zenye kujenga kunaweza kusababisha mtu kugeukia madawa ili aweze kupambana au kukubaliana na hali halisi ya maisha, kwa mfano unakuta kijana kasoma masomo ya juu kwa mda mrefu na kwa gharama kubwa na baadae anarudi mitaani na ajira hamna na pengine hawezi kufanya biashara ndogo ndogo au biashara haziendi badala yake ugeukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

4. Kuwepo kwa madawa ya kulevya kwenye jmazingira yaliyotuzunguka.

Ikiwa madawa yanapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu, uwezekano wa kutumia huongezeka kwa sababu wengine upenda kutumia kama kujaribu na mambo kama hayo.

5. Mazingira yaliyotuzunguka na kutulea.

a yenyewe kusababisha matumizi ya madawa ya kulevya kwa sababu wanaokua na kuyaona uona ni kitu cha kawaida hasa hasa

 Kukulia katika familia au jamii inayotumia madawa huongeza hatari ya kuiga tabia hiyo hasa kwa vijana ni hatari zaidi hasa like kipindi cha kutaka kujaribu kila kitu kusababisha kujaribu na kutumia dawa za kulevya kwa sababu zipo kwenye mazingira yao ya kila siku na vile vile wanaona watu wanaotumia.

 

 

6. Ukosefu wa Elimu kuhusu madawa ya kulevya.

 Kutokuwa na elimi sahihi kuhusu madhara ya madawa hufanya mtu asiogope kuyatumia na pengine walio wengi kutumia kwa sababu hawajui hasara za madawa ya kulevya,kwa hiyo ni vizuri kabisa kutoa elimu kuhusu madhara ya kutumia madawa ya kulevya.

7. Matumizi ya dawa za kulevya kwa matibabu bila usimamizi .

 Baadhi ya watu huanza kutumia dawa kama vile painkillers kwa ajili ya maumivu, kisha huwa tegemezi.

Ni vizuri kabisa jamii na watu kwa ujumla kufahamu kwamba madawa ya kulevya ni hatari na pia yanaweza kusababisha kuzima ndoto zetu na vijana wetu, na pia elimu itolewe kwenye jamii kuhusu madhara ya madawa ya kulevya.

 


Luguli Healthcare Tips

Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.