Vyakula vya kutumia kwa wagonjwa wenye shinikizo la juu la damu (High Blood Pressure)
Shinikizo la juu la damu ni hali inayohatarisha afya, ambapo mishipa inayosafirisha damu huwa nyemba hali ambayo kusababisha moyo kusukuma damu kwa nguvu ( high pressure) hali ambayo kusababisha shinikizo la damu kuwa juu , pamoja na hayo lishe bora inaweza kusaidia kudhibiti tatizo hili. Hapa chini ni vyakula muhimu kwa mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu:
1. Matunda mbali mbali usaidia katika kurekebisha shinikizo la juu la damu na pia usaidia kwenye figo na kuweka kiwango cha sukari katika hali yake matunda yenyewe ni kama ifuatavyo.
Matunda yenye potasiamu nyingi:
· Ndizi (banana) - husaidia kupunguza athari za sodiamu
· Machungwa na maji ya machungwa
· Tikiti maji (watermelon)
· Embe (mango)
· Parachichi (avocado)
· Papai (pawpaw)
· Fenesi (pineapple)
Matunda mengine yanayofaa:
· Tufaha (apples)
· Zabibu (grapes)
· Berries (raspberries, strawberries) - zina antioxidants .
matunda yenyewe yanapaswa kutumiwa kwa kiasi ili kuweza kukidhi mahitaji yawe kwa kiasi na kwa mda maalumu kadri nitakavyoweza kutoa mwongozo hapo baadae kwa sababu kila kitu kinapaswa kuwa na kiasi. Pamoja na matumizi ya matunda na pia ushauri kutoka kwa daktari na wataalamu wa afya ni muhimu na wa kufaa kanisa.
2. Matumizi ya mara kwa mara ya mboga za majani na mboga nyingine ni muhimu kwa wagonjwa wa shinikizo la juu damu kama desturi yetu ya mboga za majani ni dawa, mboga zenyewe ni kama ifuatavyo.
· Spinachi
· Sukuma wiki
· Kabichi
· Brokoli
· Figili (beetroot) - husaidia kuongeza nitrojeni oksidi kwenye damu
· Karoti
· Nyanya
· Vitunguu saumu -husaidia kupunguza shinikizo la damu
· Vitunguu maji
· Pilipili hoho
Kwa kawaida mgonjwa anapaswa kutumia mboga za majani kwa sababu ya madini yaliyomo usaidia kutanua mishipa au inafanye relaxation of blood vessels.
3. Nafaka zisizosafishwa (Whole grains)
· Shajiri (barley)
· Oats (uzi)
· Mchele mweusi au mgawanyiko (brown rice)
· Mkate mweusi (brown bread)
· Kiazi kikuu (sweet potatoes)
· Mahindi mgawanyiko (maize porridge)
4. Nyama konda na samaki
· Samaki hasa wenye mafuta kama: dagaa, ngede (mackerel), samaki waji (salmon) - yana Omega-3
· Kuku mweusi (kondoo) asiye na ngozi
· Nyama ng'ombe konda (lean beef kwa kiasi)
· Inge (beans) na mbaazi (lentils) - badala ya nyama
5. Bidhaa za maziwa zenye mafuta kidogo
· Maziwa yaliyopunguzwa mafuta (low-fat)
· Mtindi (yoghurt) usio na sukari
· Jibini la mafuta kidogo (kwa kiasi cha wastani)
6. Matumizi ya karanga na mbegu.
· Maharage ya soya
· Karanga (peanuts) - zisizo na chumvi
· Alizeti (sunflower seeds)
· Lozi (almonds)
· Korosho (cashews)
· Ufuta (sesame seeds)
7. Mafuta yenye afya
· Mafuta ya zeituni (olive oil)
· Mafuta ya alizeti (sunflower oil)
· Mafuta ya nazi (coconut oil) kwa kiasi
· Mafuta ya kitunguu saumu.
Tunapaswa kufahamu kwamba vyakula vilivyoandika hapo ni vya kutumia kwa mgonjwa wa shinikizo la juu la damu ila na mgonjwa anapaswa kuzingatia maagizo ya daktari pamoja na kuudhuria klinick na pia matumizi ya dawa ni muhimu kwa wale walioanza dawa tayari.
Luguli Healthcare Tips
Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.