Habari za Afya

Fahamu kuhusu ugonjwa wa homa ya ini na Aina zake

Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa homa ya ini na Aina zake kama tutakavyoona hapo chini.

Homa ya ini  ni ugonjwa ambao kwa dada hivi unashambulia watu wengi na kwa kasi kwa kuonyesha dalili za moja kwa moja au kutoonyesha dalili kabisa.

Ugonjwa wa ini ni hali ya kuvimba kwa tishu za ini. Uvimbe huu husababisha seli za ini kushindwa kufanya kazi zake vizuri, jambo ambalo linaweza kusababisha uharibifu wa kudumu (cirrhosis) au kansa ya ini ikiwa hautatibiwa.

​Ingawa inaweza kusababishwa na pombe au sumu, mara nyingi husababishwa na virusi. Kuna aina tano kuu za virusi vya homa ya ini

​Aina za Homa ya In

​Hepatitis A ,Huenezwa kupitia ulaji wa chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi cha mtu mwenye maambukizi. Mara nyingi ni ya muda mfupi na haisababishi ugonjwa sugu na pengine huweza kupona kabisa.

​Hepatitis B, Huenezwa kupitia damu, majimaji ya mwili (kama mate au shahawa), na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Hii inaweza kuwa sugu na kusababisha madhara makubwa ya muda mrefu

​Hepatitis C ,Huenezwa zaidi kupitia mgusano wa damu na damu (kama kuchangia sindano au vifaa ncha kali). Mara nyingi huanza bila dalili na kuwa ugonjwa sugu wa ini

​Hepatitis D ,Aina hii ni ya pekee kwa sababu inaweza kumpata mtu ambaye tayari ana Hepatitis B pekee. Huongeza hatari ya ini kufeli haraka

​Hepatitis E  Kama ilivyo aina A, huenezwa zaidi kupitia maji na chakula kichafu. Ni hatari zaidi kwa akina mama wajawazito

 


Luguli Healthcare Tips

Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.