PPH ni upotezaji wa damu nyingi kupita kiasi (zaidi ya 500ml kwa uzazi wa kawaida au zaidi ya 1000ml kwa upasuaji) ndani ya saa 24 baada ya kujifungua.
Hizi hapa ni sababu kuu nne zinazofahamika kitaalamu kama "The 4 Ts":
1. Tone (Ulegevu wa Uterus) — Inasababisha 70% ya PPH
Hii hutokea wakati misuli ya mfuko wa uzazi (uterus) inaposhindwa kujikaza (contract) baada ya kondo la nyuma kutoka. Kazi ya contractions ni kubana mishipa ya damu ili kuzuia uvujaji.
Sababu: Uchungu wa muda mrefu sana, kubeba mapacha, mtoto mkubwa sana, au kuwa na maji mengi ya uzazi (polyhydramnios).
2. Tissue (Mabaki ya Tishu)
Hii hutokea wakati sehemu ya kondo la nyuma (placenta) au mabonge ya damu yanapobaki ndani ya mfuko wa uzazi. Mabaki haya yanazuia uterus kujikaza vizuri, hivyo damu inaendelea kuvuja.
3. Trauma (Majeraha)
Uharibifu wa njia ya uzazi wakati wa mchakato wa kusukuma mtoto.
Mifano: Kuchanika kwa mlango wa uzazi (cervix), uke (vagina), au msamba (perineum). Hata kupasuka kwa uterus (uterine rupture) kunaangukia hapa.
4. Thrombin (Matatizo ya Mgando wa Damu)
Hii ni nadra zaidi. Inatokea wakati damu ya mama inaposhindwa kuganda vizuri ili kuziba jeraha la kondo la nyuma. Hii inaweza kusababishwa na matatizo ya kurithi au hali kama pre-eclampsia kali.
Luguli Healthcare Tips
Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.