Hatua Zinazochukuliwa na Madaktari na watumishi wa afya kwa Mama anayetokwa na Damu nyingi.
Ikiwa PPH inatokea, timu ya matibabu hufanya yafuatayo haraka:
Masaji ya Uterus
Kusugua tumbo la mama kwa nje ili kuchochea uterus ijikaze.
Dawa
Kutoa dawa kama Oxytocin, Misoprostol, au Ergometrine ili kusaidia uterus kusinyaa.
Kuongezewa Maji/Damu:
Ili kurudisha kiasi cha damu kilichopotea na kuzuia "shock".
Upasuaji mdogo au mkubwa
Ikiwa dawa zimeshindwa, daktari anaweza kuingiza mkono kutoa mabaki ya tishu au kufanya upasuaji kuzuia uvujaji.
Kumbuka: PPH inaweza kutokea ghafla hata kwa mama ambaye hakuwa na viashiria vyovyote vya hatari. Ni muhimu sana kujifungulia kwenye kituo cha afya chenye wataalamu.
Luguli Healthcare Tips
Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.