Magonjwa Makuu katika Kipindi cha Neonatal
Maambukizi ya Bakteria (Neonatal Sepsis): Haya ni maambukizi yanayoingia kwenye damu ya mtoto. Ni hatari sana kwani yanaweza kusambaa haraka mwilini.
*
Matatizo ya Kupumua (Respiratory Distress Syndrome): Hali hii huwapata watoto waliozaliwa kabla ya muda (preterm) kwa sababu mapafu yao hayajakomaa kutengeneza surfactant.
Manjano (Neonatal Jaundice): Hali ya ngozi na macho kuwa ya njano kutokana na kiwango kikubwa cha bilirubin damuni, mara nyingi kwa sababu ini la mtoto bado ni changa.
*
Maambukizi ya Kitovu (Omphalitis): Hii ni hali ya kitovu kuambukizwa na bakteria, jambo linaloweza kusababisha sepsis ikiwa halitashughulikiwa.
Hypoglycemia (Sukari ya chini): Hali hii hutokea kwa watoto waliozaliwa na mama wenye kisukari au walio na uzito mdogo, na inaweza kusababisha kifafa au madhara ya ubongo.
Ufuatiliaji na Uingiliaji Kati wa Uuguzi
Kama mwanafunzi wa uuguzi, ni muhimu kusisitiza kuwa ishara za hatari (kama mtoto kukataa kunyonya, kupumua kwa shida, au homa/baridi) si lazima ziwe na dalili dhahiri za ugonjwa mmoja. Mara nyingi, mtoto anaweza kuonekana "hapana sawa" tu. Uchunguzi wa kimwili wa mara kwa mara na vipimo vya maabara (kama Full Blood Picture au blood culture) ni muhimu sana.
Luguli Healthcare Tips
Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.