Madawa ya kulevya ni janga ambalo lipo katika jamiii zetu na pia kuna watu wengi walitumia na baadae waliweza kuacha na kurudi kwenye hali yao ya kawaida ingawa mbinu na mikakati mbali mbali inahitajika ili kumtoa mtu kwenye kitu alichokizoea na akidai kwamba kinamletea nafuu ya maisha na kimrudisha kwenye uhalisia wa maisha.zifuatazo ni mbinu za kupambana na madawa ya kulevya.
1. Uhamasishaji na uelimishaji wa jamii.
Kutoa elimu kwa vijana na jamii kuhusu madhara ya kisaikolojia, kiafya na kijamii ya madawa. Shule, misikiti, kanisa na vyombo vya habari vinaweza kuwa vyombo vya kufikia ujumbe huu.
2. Kufunga njia za upatikanaji wa madawa ya kulevya.
Kuimarisha usalama mipakani, kukabiliana na biashara haramu za madawa, na kufunga duka za dawa zisizoruhusiwa. Pia, kudhibiti uagizaji na usambazaji wa kemikali zinazotumika kutengeneza madawa.
3. Adhabu, mikakati na sheria kuzingatiwa.
Kutekeleza sheria kali dhidi ya wauza madawa na wanaosafirisha, pamoja na kuhakikisha mahakama zinachukua hatua za haraka na zenye nguvu.
4. Huduma za ushauri kwa wahangwa. Kuanzisha vituo vya kulevya (rehabilitation centers) vinavyotoa matibabu, ushauri wa kisaikolojia, na msaada wa kujiondoa kwenye uraibu. Pia, kuwa na programu za ufuatiliaji baada ya matibabu.
5. Kushirikisha jamii na familia – Kuwawezesha wazazi na viongozi wa jamii kutambua dalili za mapema za matumizi ya madawa, na kujenga mazingira salama ya kuzuia na kusaidia walioathirika.
6. Kuwepo kwa mahitaji muhimu kwa jamii
Kuunda fursa za ajira, michezo, sanaa na burudani zenye kujenga kwa vijana, ili kupunguza uvivu na kuvutia akili zao kwenye shughuli chanya.
7. Ushirikiano wa kimataifa na kitaifa.
Kushirikiana na nchi jirani na mashirika kama UNODC (Ofisi ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Madawa na Uhalifu) kwa kubadilishana taarifa na kukamata usafirishaji wa madawa.
Mbinu hizi zikitekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali, jamii, wazazi, na vijana wenyewe, zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la madawa ya kulevya.
Luguli Healthcare Tips
Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.