Habari za Afya

Vyakula vya kuepuka kwa wagonjwa wa shinikizo la damu

Post hii inahusu zaidi vyakula vya kuepuka kwa wagonjwa wa shinikizo la damu

Shinikizo la juu la damu au kwa lugha ya kawaida ni presha ya kupanda,ni pale ambapo presha inakuwa juu ya kiwango cha kawaida kadri ya vipimo kutoka kwa wataalamu wa afya,mgonjwa akishagunduliwa na kuambiwa kwamba presha yake ipo juuu anapaswa kujiepusha na vyakula mbali mbali kama hapo tutakavyoona kwenye maelezo ya chini.

 

1. Chumvi kupita kiasi.

 Vyakula vilivyowekwa chumvi nyingi sio salama kwa mgonjwa wa presha kwa sababu vyenyewe vina tabia ya kupandisha presha kama mgonjwa ana presha tayari ni hatari vyakula hivyo ni kama vitafunwa (crisps, snacks), vyakula vya makopo (supu, mboga), nyama chumvi (sausage, bacon, salami), na samaki kavu.Na pia tunapaswa kufahamu kwamba sio kila mgonjwa wa presha hapaswi kutumia chumvi kabisa anatumia kidogo na pia kufuata maagizo ya daktari.

2. Mafuta yaliyojaa na mafuta ya trans haya ni mafuta ambayo kwa kawaida uongeza presha kwa hiyo kwa wagonjwa wa presha hawapasei kutumia mafuta haya  , Kama vile kukaanga (chips, samaki kukaanga), nyama nyekundu yenye mafuta, siagi, jibini, na mafuta ya nguruwe (margarine) na pia ushauri wa daktari inahitajika kufahamu ni mafuta ganu yasitumiwe na mgonjwa wa presha.

3. Vinywaji vyenye sukari nyingi – Soda, juisi za matunda zilizoongezwa sukari, na vinywaji vya nishati.

4. Pombe – Pombe nyingi huongeza shinikizo la damu; punguza kiasi au epuka kabisa.

5. Vyakula vyenye sodiamu nyingi – Mchuzi wa soya, mchuzi wa nyama, viungo vya kujikita (stock cubes), na vyakula vya haraka (fast food).

6. Maziwa yenye mafuta kamili – Kama maziwa ya ng’ombe yasiyokolezwa (full cream), yoghurt nzito, na cream.

Ka hiyo sio kila kilichoandikwa hapo juu hakipaswi kutumiwa kabisa na mgonjwa wa shinikizo la juu la damu hapana, vyakula hivyo vinaweza kutumka kwa kiwango kidogo kwa sababu pamoja na kuwepo kwa shinikizo la juu la damu na kuna vyakula vina nafasi yake kwenye mwili wa binadamu,kwa hiyo ushauri wa daktari ni muhimu katika kuchagua vyakula vya kutumia.

 

 

 

 


Luguli Healthcare Tips

Kumbuka kutembelea kliniki yetu Buguruni kwa ushauri zaidi wa kitaalamu kuhusu afya yako. Afya yako ni jukumu letu.